Wednesday, 3 September 2014

USAFIRI SIO ISHU


Natumaini umeshasikia majina kama usafiri,nyuma,kujazia,mnye,mkia na mengine mengi yakisifia makalio kwa wanawake.
Binafsi nimezoea kuona kua wanawake wana makalio makubwa zaidi ya wanaume na nimekua nikiamini ndio kawaida,hata tukiona mwanaume ana makalio makubwa huwa kama tunashangaa na kwake huwa ni kero, utafiti uliofanyika hivi karibuni huko ujerumani na Preininger B. et al katika pepa yao "The sex specificity of hip-joint muscles offers an explanation for better results in men after total hip arthroplasty" unaonesha kua wanaume ndio wana "ujazo mkubwa wa misuli ya makalio" kuliko wanawake.
Hii inaendana kabisa na ukweli kuwa wanaume huwa wana misuli mikubwa kuliko wanawake.
Je, kile tunachokiona kwa wanawake ni nini sasa? Hayo ni mafuta.
Katika kitabu kinachoitwa Text book of medical physiology kilichoandikwa na Arthur C.Guyton kinaeleza kuwa kuongezeka kwa kiasi cha mafuta mwilini kunapunguza usisimuliwaji wa seli na sukari kwenye damu,swala ambalo linapelekea kisukari,
sio tu hivyo,mafuta mengi mwilini huusishwa na magonjwa kama shinikizo la dam na saratani.Kuna haja ya kubadili mtazamo sasa, naamini hii inawezekana maana historia inatuambia mwanamke mzuri katika roma ya mwanzo alikua ni mwanamke mnene,ila leo huko magharibi mwanamke mnene ni kero. Wanaume wabadili tabia na wasiyaone makalio makubwa sana kama mazuri sana.
simaanishi wasiyaone makalio kama uzuri wa mwanamke hapana,makalio yanawafanya wanawake waonekane wazuri ila yasiwe malaini yenye mafuta mengi.
Wanawake wafanye mazoezi ili wapunguze mafuta na wakuze misuli ya makalio,hapo yatakua mazuri zaidi yenye kuvutia.

By Joseph Julius Masalu ( MD4,MUHAS)

Share this

2 Responses to "USAFIRI SIO ISHU"

  1. We have to learn more from the grass root

    ReplyDelete
  2. Qn is why women....?does estrogen have any effect on distribution of fats in women?

    ReplyDelete